+255754692056
info@standardvoice.co.tz
Facebook
Twitter
Instagram
logo2transperantlogo
  • Home
  • About Us
  • Standard Radio
    • Programs Line Up
  • Connectivity to Community
  • Our Team
  • Contact

Standard Radio

Home Standard Radio

UZINDUZI WA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO

IMG_8715

Wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo wameshuhudia uzinduzi wa mpango mkakati wa miaka mitano wenye lengo la kuchochea mabadiliko ya kilimo Read More

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda ambae ametaka kuwepo kwa kilimo cha kisasa na cha umwagiliaji ambacho kitaweza kuwatoa wakulima katika umaskini.

Kwa upande wao, baadhi wa wadau wa sekta hiyo, wameonyesha shauku ya kutaka utekelezwaji wa mkakati huo kufanyika kwa ufanisi ili uweze kuleta tija.

Uzinduzi wa mkakati huu, unakuja wakati ripoti ya Umoja wa Mataifa ikionyesha wasiwasi wa kutofikiwa kwa baadhi ya malengo ya Maendeleo Endelevu ya dunia kufikia mwaka 2030.Hata hivyo, baadhi ya wadau hao waliohudhuria uzinduzi huo uliofanyika jijini Dodoma wamesema, mabadiliko yanaweza kupatikana iwapo tu utekelezaji wa mikakati hiyo utafanyika kwa ufanisi.

Huu ni mkakati wa tatu kuzinduliwa nchini, ambapo tofauti na ile iliyopita ambayo ilijikita zaidi katika kujenga mifumo ikiwemo utengezaji wa mbegu bora pamoja na kutoa elimu kwa wakulima

KITUO CHA SHERIA ( LHRC ) IMEWATAKA WALIOTISHIWA MAISHA WATOE TAARIFA POLISI

IMG_8650

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimekemea vikali matukio ya kutishiwa maisha kwa baadhi ya Watanzania wanaoonekana kuwa na mlengo au maoni tofauti Read More

Sambamba na hilo, LHRC imekemea vitendo vya baadhi ya viongozi wa Serikali hususani mawaziri kutoa maonyo ambavyo yanaashiria kuwatishia Watanzania wanaotekeleza uhuru wao wa kutoa maoni kupitia majukwaa mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamli.

Katika taarifa ya kituo hicho iliyotolewa imeeleza kuna malalamiko ya watu wanaotishiwa maisha yao na watu wasiojulikana kwa sababu maoni yao yanakinzana na yale ya upande mwingine hasa kwenye mijadala inayohusu maslahi mapana ya Taifa.

Taarifa hiyo ambayo imesainiwa na Mkurugenzi MKuu wa LHRC, Anna Henga imeeleza kwa takribani juma moja sasa imepita ambapo kumekuwa na mjadala wa baadhi ya Watanzania kulalamika kutishiwa maisha yao na watu waliodai wasiojulikana kutokana na misimamo yao kwenye mambo mbalimbali yanayogusa masiahi ya umma.

Kufuatia hilo, LHRC imewataka watu wote waliopokea vitisho kutoa taarifa kwa Polisi ili hatua zichukuliwe ikiwa pamoja na upelelezi ili wahusika wajulikane na wafikishwe mbele ya sheria.Pia, imeitaka Serikali kulinda, kuhifadhi na kuheshimu uhuru wa Watanzania kutoa maoni yao kwa mujibu wa sheria sambamba na uhuru wa kukusanyika

HAKUNA BANDARI INAYOUZWA TANZANIA- PAULINE GEKUL, NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA.

bebdcaa0-9069-4d29-96e6-12cc3500f7e5

Naibu waziri wa Katiba na Sheria ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Pauline Gekul amesema hakuuna bandari inayouzwa kutokana na kuwepo kwa uvumi wa kuuzwa kwa bandari Read More

Naibu Waziri Gekul ameyasema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa kata ya nangara ziwani iliyopo kwenye Jimbo lake la Babati mjini ikiwa ni Katika muendelezo wa wa ziara yake ya kuzungumza na Wananchi kwenye Jimbo lake.

Akiwa katika ziara hiyo pamoja na mambo mengine Gekul ameendelea kusisitiza kuwa Hakuna bandari ya iliyouzwa kwa kuwa serikali imefungua milango ya kuendelea kutoa fursa kwa wananchi kuendelea kutoa maoni Yao huku serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ikiwa inaendelea kufanyia kazi maoni hayo.

Sanjari na hayo mbunge Gekul Akizungumzia maendeleo Katika Jimbo lake kupitia ziwra hiyo , amewasihi Wananchi wa Kata ya nangara ziwani kujitahidi kuchangia kwa kushirikiana na serikali ili kujjenga shule nyingine ya sekondari Katika kata hiyo.

Aiha ameongeza kuwa pamoja na shule ya sekondari pia Wananchi wa wa kata hiyo wanatikiwa pia Kushiriki Katika kufanikisha ujenzi zahati katika Kata hiyo kutokana na ongezeko la watu ili kuboresha huduma ya Afya

TAKWIMU ZA MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI NDIO CHACHU YA MIPANGO YA MAENDELEO

IMG_8593

Imeelezwa utoaji wa mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa wadau na viongozi mbalimbali wa utawala yatasaidia kuwajengea uwezo viongozi kutekeleza majukumu yao kwa kuwatumikia wananchi katika jamii kwa kutumia takwimu hizo Read More

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya halimashauri ya manispaa ya singida mheshimiwa paskasi muragili katika semina iliyoandaliwa na halmashauri ya singida vijijini na manispaa ya singida iliyolenga kutoa mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa  kwa viongozi wa  serikali 

Aidha mkuu wa wilaya muragili ameeleza dhamira ya serikali kutoa mafunzo hayo kuwa lengo ni kusaidia viongozi wote kuanzia ngazi mbalimbali za kiserikali  katika kufanya maamuzi, kutathimin na kupangilia mipango ya maendeleo

Katika hatua nyingine muragili ameipongeza serikali ya awamu ya sita iliyochini ya raisi dk samia suluhu hassan kufanikisha zoezi hilo na kuwa miongoni wa nchi zinazopigiwa mfano katika utekelezaji wa mpango wa umoja wa mataifa wa utekelezaji wa sensa katika mzunguko wa mwaka 2020

Sambamba na hayo muhandisi muragili amesisitiza umuhimu wa matumizi ya mafunzo hayo kwa viongozi walioshiriki semina hiyo kuyatumia katika kutatua kero zinazowakabili wanachi katika maeneo yao kwa kuzingatia uhitaji umbali na kiasi cha huduma zilizopo

Kwa upande wake katibu tawala mkoa wa singida mh dk fatma mganga amewataka mafisa mipango na watendaji wa kata na vijiji kuhuisha bajeti za mipango ya maendeleo kwa kutumia takwimu sahihi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi mipango ambayo itakua na tija kwa wananchi


RAIA WA UKRAINE ASHTAKIWA KWA KUSAFIRISHA KOBE 116 NCHINI TANZANIA

IMG_8091

Raia wa Ukraine, Orga Kryshtopa amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kusafirisha kobe 116 wenye thamani ya Sh18.9 milioni bila kibali.Read More

Mashitaka ya Kryshtop yalisomwa katika mahakama hiyo jana Juni 21, na Wakili wa Serikali, Judith Kyamba, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Amir Msumi.

Kabla ya kusomewa mashtaka yake, Hakimu Msumi alimweleza mshtakiwa huyo kuwa hatakiwi kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi isipokuwa kwa kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Akisoma mashitaka hayo, Wakili Kyamba alidai kuwa katika shtaka la kwanza kati ya Januari 20 na Julai 30, 2022 jijini Dares Salaam, mshtakiwa alihusika katika kununua, kuuza na kusafirisha kobe 116 wenye thamani ya Sh18.9 milioni mali ya Serikali ya Tanzania.

Katika shtaka la pili, inadaiwa tarehe hizo hizo, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Kryshtopa alikamatwa na kobe hao bila kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori Tanzania.

Upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, hivyo umeomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Msumi ameahirisha kesi hiyo hadi Juni 28, 2023, ambapo upande wa mashtaka unatarajia kuongeza mshtakiwa mwingine. Mshtakiwa amerudishwa rumande hadi tarehe hiyo.

 

TANZANIA KUTUMIA SH2.9 TRILIONI KWA ULINZI KATIKA BAJETI IJAYO

IMG_6493

Bunge limeidhinisha bajeti ya Sh2.9 trilioni kwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mwaka wa fedha wa 2023/24 Read More

Waziri wa Ulinzi, Innocent Bashungwa, akiwasilisha bajeti hiyo, alisema Sh2.767 trilioni zitakuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh222.8 bilioni zitatumika kugharamia miradi ya maendeleo.

Miongoni mwa vipaumbele vya juu katika bajeti hiyo ni kujenga uwezo na kuendeleza miundombinu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili kuchukua vijana wengi zaidi kwa ajili ya kukuza ujuzi.

Bw. Bashungwa alitaja maeneo mengine ya kipaumbele, kama vile ununuzi wa silaha na zana za kijeshi zinazoendana na maendeleo ya teknolojia na mawasiliano, katika azma ya kuboresha mazingira ya kazi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Aliongeza kuwa wizara hiyo pia itaimarisha mashirika na taasisi za utafiti wa kijeshi, ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda vya ulinzi kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa na huduma kwa ajili ya majeshi na wananchi.

Wizara pia itaimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili na mashirika ya kimataifa, ya bara na ya kikanda kama vile Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika katika nyanja za ulinzi na usalama.

MOMONYOKO WA MAADILI

IMG_4771

Ameongeza kwamba ndoa zilizofarakana,malezi ya watoto yatakuwa duni au hakuna kabisa. Watoto wanatembea kama kuku wa kienyeji.

“Lakini ndoa zikiwa imara,watoto watalelewa inavyotakikana.Na malezi hayo watawafanya watoto kuwa na tabia njema.Hawawezi kudanganyika kirahisi wakaanza kuingiliana kinyume na maumbile,kusagana au kulawitiana”,amefafanua.Read More

Ameongeza zaidi kwamba vitendo hivyo havitakubalika kabisa. Kwa sababu vipo kinyume na utamaduni,mila zetu za asili na Mungu havipendi.

“Tusikubali kuburuzwa kwamba vitendo hivyo,ni haki ya kibinadamu.Mnyama ngamia hafanyi mapenzi na ngami wa ukoo moja.Vile vile simba naye hawezi kufanya mapenzi na simba wa ukoo.Simba dume mdogo,hufukuzwa na simba dume mkubwa, na kwenda mbali zaidi”amesema mbuge Mtaturu.

Aidha,amesema endapo tutakomesha momonyoko wa maadili,tutaipa serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan,nafasi ya kuendelea kuwaletea wananchi maendeleo katika  sekta mbali mbali.

Mbunge Mtaturu,ametumia nafasi hiyo kuipongeza BAKWATA mkoa wa Singida,kwa uamuzi wake wa kutenga ‘usiku wa staha’.Siku hiyo  inatumika kutathimini mila na utamaduni wa asili,kama unaenda vizuri.

Naye mbunge mstaafu bunge la Afrika mashariki,Josephine Lemanyan,alisema tusipoambizana ukweli kwamba huko tunakoelekea,tutajikuta tumeingia kwenye vitendo vya kusagana,kulawitiana na kuingiliana kinyume na maadili.

Alisema hayo yakitendeka,taasisi za ndoa nyingi zitavunjika.Wanawake watakuwa wanavaa mavazi ya ajabu na ya aibu.Tudumishe utamaduni wetu.Wanaume/wanawake, warejee kuvaa nguo za staha.

Sheikh wa wilaya ya Singida mjini,Issa Simba,alisema kuna kipindi kesi za kuachana/kutalikiana wana ndoa,zilizindi mno.

“Hali hiyo ilitusukuma kuanzisha vikao vya ‘usiku wa staha’.Hiki cha mwaka huu, ni kikao cha tano.Tunapokutana,huwa tunatathimini endapo kasi ya wanaume na wanawake kuachana,imeongezeka au imepungua.Kama imeongezeka,tunatafuta dawa ya kutokomeza”,amesema.

Mtemi Ahmed Misanga,amewataka waumini wa madhehebu mbalimbali ya dini na wasio waumini lakini wana uwezo.Wajenge utamaduni wa kusaidia kwa hali na mali,jamii isiyo na uwezo.Ili kuwapunguzia makali ya maisha.

MWANAMKE APIGWA VIBOKO KWA TUHUMA ZA KUIBA SHILINGI LAKI NNE NA ELFU ISHIRINI

IMG_4667

Akizungumza na Vyombo Vya Habari Mwanamke huyo amesema kuwa  tukio lilitokea Aprili 14 majira ya saa sita usiku wakati akitimiza majukumu yake ya kikazi katika  baa na nyumba ya kulala wageni ndipo  mwanaume anayefamika  kwa jina la Julias Marimo  aliyekuwa akimtaka kimapenzi akamuomba ampelekee shuka chumbani, wakati akitimiza majukumu ya mteja huyo ndipo Marimo alifika  chumbani na kudai kuwa amepoteza  kiasi hicho Cha fedha  huku akimtuhumu Manka kuwa wameiba fedha hizo .Read More

Wakati akielezea tukio Hilo Manka anasema kuwa baada ya pulungushani hizo kesho yake alipelekwa kwa Jeshi la Jadi Sungusugu ambapo hakupata msaada  na badala yake alipigwa viboko vilivyomsababishia maumivu na kupelekwa Hospitali ya Rufaa  Mkoa wa Shinyanga kwaajili ya matibabu.

Kwa upande wake Muuguzi wodi namba Saba katika Hospital hiyo Welu Kiwura amesema mgonjwa alifikishwa  Hospitali  akiwa na maumivu sehemu mbalimbali za mwili wake. Afisa Usitawi wa Jamii Hospitali ya Rufaa Mkoa wa shinyanga prisila Mushi akisema tukio Hilo ni la kikatili na kuiomba Serikali kukomesha hali hiyo.

Kamanda wa Jeshi la  Polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi amekili kutokea kwa tukio Hilo huku akiihakikishia Jamii ya Shinyanga kuwa Jeshi la Polisi  Mkoa wa Shinyanga watahakikisha wanawatia hatiani wahusika wa tukio Hilo ili Sheria ichukue mkondo wake.

SERIKALI MKOANI SINGIDA KUCHUKUA HATUA KWENYE VITENDO VYA KUINGILIANA KINYUME NA MAUMBILE

IMG_4629

Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan,inatambua kwamba malezi mema ni maandalizi ya watoto kuja kuwa waadilifu na wenye hofu ya Mungu.Hivyo upo umuhimu mkubwa watoto wakapewa malezi na elimu bora,ili waweze kutambua madhara ya kuingiliana kinyume na maumbile,usagaji pia kuuza miiili yao”,amefafanua zaidi Read More

Awali katibu BAKWATA mkoa wa Singida,Alhaj Buruhani Mlau,aliwaasa wazazi wadumishe malezi rafiki kwa watoto wao,ili watoto wawe na ujasiri wa kueleza taarifa endapo watafanyiwa vitendo viovu.

Alhaj Mlau alisema wapo baadhi ya wazazi wanakuwa na ukali uliopitiliza kwa watoto wao.Kitendo hicho kinachangia watoto  kuongopa kutoa taarifa kuhusu  vitendo ambavyo vipo kinyume na sheria.

Pia alhaj Mlau,amewataka wanawake wawalinde na kuwatunza  vizuri watoto wao,ili waje kuwa jamii yenye maadili mema.

“Wanawake jengeni utamaduni wa kutenga muda wa kukaa na watoto weno wakiwemo wa kike.Wasikilizeni vizuri na wapeni elimu bora ya wao kujilinda dhidi ya vitendo vitakayochangia maisha yao kuharibika”,alisema Alhaj Mlau.

Kwa upande wake mzee maarufu manispaa ya Singida,Juma Mudida,alisema vitendo hiyo vya kuingiliana kinyume na maumbili,kwenye vitabu takatifu,vimepinga marufuku watu kujihusisha navyo.

Alisema vitendo hivyo vina madhara mengi ikiwemo mhusika kutokwa na choo ovyo bila utaratibu.

Aidha,mzee Mudida alisema upo umuhimu sheria zinazohusu vitendo hivyo,ikaangaliwa upya ili pamoja na mambo mengine,kuongeza makali zaidi.Ikiwezekana kutunga sheria endapo mtu atabainika,apewe adhabu ya kifo.

Mkutano huo maalum,uliandaliwa na BAKWATA mkoa wa Singida,na ulifanyika katika kituo cha mabasi cha zamani mjini Singida.Lengo la mkutano huo,lilikuwa kulaani na kupinga vita vitendo vya kuingiliana kinyume na maadili,ushoga na usagaji.

SERIKALI KUPUNGUZA MFUMKO WA BEI , SINGIDA.

IMG_4478

Mwenyekiti huyo ambaye ana miaka 40 toka awe mfanyabishara wa kuku wa kienyeji,amesema hajawahi kukubwa na kipindi kigumu kama cha sasa,cha kukosa wateja.

“Kipindi kama hiki cha kuelekea kwenye siku kuu au sherehe,tulikuwa tunashafirisha Dar-es-salaam, kuku kwenye malori,kati ya mbili  na tatu kwa siku tatu mfululizo.Siku hizo sasa zimebaki kuwa historia”,amesema mwenyekiti huyo.Read More

Amefafanua kuwa  siku hizi wamerudi kwenye mpango wao wa zamani wa  kusafirisha kuku kila jumapili na jumatano.Na lori zingine  nyingine wanashindwa kuzijaza.

Mwenyekiti huyo,ametumia fursa hiyo kuiomba manispaa ya Singida,kujenga utamaduni wa kukitembelea kikundi hicho mara kwa mara.Ili waweze kusaidia kutatua changamoto pindi zinapowakabili.

Katibu wa kikundi hicho,Jumanne Rajabu maarufu kwa jina la Word,alisema maisha ya Mtanzania wa sasa,ni magumu kupindukia.Na huko kumechangiwa na mfumko wa bei.

“Huko nyuma mchele kilo moja ulikuwa ukiuuzwa kati ya shilingi 1,900 na 2,000.Sasa hivi mchele unauzwa kilo moja  kati ya shilingi 3,500 na 4,000.Ukinunua kuku mmoja,ukanunua na mafuta na vikombolezo mbali mbali,kama una familia kubwa,msosi wa siku moja, utakugharimu zaidi ya shilingi 40 alfu.Watu wa hivyo wamebakia wachache mno”,alifafanua.

Kwa upande wa biashara ya kuku wa kienyeji,alisema kuwa biashara hiyo haijapona,imeathiriwa na mfumko wa bei.Walaji wa kuku wamebakia wachache mno.Kuku sasa amekuwa anasa.

Word ambaye amefanya biashara ya kuku wa kienyeji kwa miaka 20,amesema kuwa huko miaka ya nyuma,walikuwa wanaingiza kipato kikubwa, hasa siku za kuelekea siku kuu au sherehe zingine.

“Nakumbuka katika kipindi hicho,mteja ukimtajia bei,wala habishi.Anatoa mara moja.Siku hizi kwenye siku ya kuelekea siku kuu,wala huwezi kuona mtu ananunua kuku.Tunatunza kuku kwenye vibanda,hadi wanajifia.Tunaiomba Serikali isaidie kutatua changamoto hiyo ya mfumko wa bei”,Word alisema.

Aidha,mfanyabiashara mwingine wa kuku wa kienyeji wa miaka minne,Mgwira Amasi,alisema kuwa kwa sasa wanaweza kumaliza siku tatu au nne,hawajauza kuku kabisa.Mwisho wanajifia tunaingia hasara.

“Zamani tulikuwa tunasafirisha kuku Dar-Es-Salaamu,wafanyabishara wa huko wanawauza halafu wanakutumia fedha.Siku hizi wanakataa mtindo huo, kwa hofu zitawaozea.Shida kubwa ni kwamba hawana watejakabisa  kama zamani”amefafanua.

Alifafanua zaidi kwamba maisha yamekuwa magumu kwa sababu hawana fedha.Na kila kitu kimepanda bei.Unga kilo 25 siku za nyuma tulinunua unauzwa shilingi 25,000.Kwa sasa ni shilingi 45,000.Na bado bei inaweze kupanda zaidi.

Naye mfanyabiashara wa nyama za ng’ombe katika soko kuu la mjini Singida,Seleman Issa,alisema Watanzania wengi hasa wa ngazi za chini,maisha yao kila kukicha,yanaendelea kuwa magumu mno.Shida kubwa ni mfumko wa bei.Mfumko wa bei upatiwe ufumbuzi wa kudumu.


URUSI INAWEZA KUPIGANA 
NCHINI UKRAINE KWA MIAKA MIWILI ZAIDI – LITHUANIA 

IMG_3045

 

Moscow inasema ilizindua “operesheni yake maalum ya kijeshi” nchini Ukraine mwaka mmoja uliopita ili kukabiliana na tishio la usalama wake. Kyiv na nchi za Magharibi zinavitaja vita hivyo kama visivyochochewa kulitiisha taifa huru. Read More

“Rasilimali ambazo Urusi inazo kwa sasa zingetosha kuendeleza vita kwa kasi ya sasa kwa miaka miwili,” mkuu wa upelelezi wa Lithuania Elegijus Paulavicius aliwaambia waandishi wa habari.

“Kwa muda gani Urusi itaendeleza vita hivyo pia itategemea uungwaji mkono wa jeshi la Urusi kutoka mataifa kama vile Iran na Korea Kaskazini”, aliongeza.

Paulavicius alikuwa akiwasilisha muhtasari wa tishio la kitaifa na mashirika ya kijasusi ya Lithuania, ambayo pia yalidai wadukuzi wanaohusishwa na serikali ya Urusi na China walijaribu mara kwa mara kuingia katika kompyuta za serikali ya Lithuania mwaka 2022.

“Kipaumbele chao kinabaki kuwa ukusanyaji endelevu wa muda mrefu wa habari zinazohusiana na mambo ya ndani na nje ya Lithuania,” mashirika hayo yalisema.

TANZANIA KUANZA KUSAFIRISHA MBOLEA NCHINI KENYA 


mbolea

Katibu wa Baraza pia aliwaahidi wakulima kwamba serikali itaendelea kutoa ruzuku ya mbolea na kuhifadhi bei kwa KSh3,500 (Tsh 65581.19) za sasa hadi suluhu ya kudumu ipatikane.Read More

Kwa kuagiza mbolea kutoka Tanzania, Linturi aliteta kuwa Kenya itapunguza utegemezi wake kwa mataifa ya Ulaya na Morocco.

”Sioni haja ya kuagiza mbolea kutoka nchi za mbali wakati tunayo Tanzania,” akasema Bw Linturi. Kwa sababu ya malighafi ya bei nafuu, na umbali kati ya Kenya na Tanzania, hii itahakikisha tunakuwa na mbolea ya bei nafuu kwa wakulima wetu,” aliongeza.Bw Linturi , alitangaza hili baada ya kutembelea Itracom , watengenezaji wa mbea ya Fomi nchini Tanzania .

Alieleza kuwa mtindo wa uzalishaji wa kampuni hiyo, unaohusisha matumizi ya mbolea ya kikaboni na fosforasi, umeonekana kuwa na uwezo wa kuongeza maradufu uzalishaji wa mazao kwa kurutubisha udongo.

“Mbolea imeongeza uzalishaji wa chakula kwa hadi asilimia 39 na kupunguza gharama za uzalishaji nchini Tanzania,” alisema.

Wataalamu wa masuala ya kilimo wamesema kuendelea kwa matumizi ya mbolea zisizo asilia ndio chanzo cha kuzorota kwa hali ya udongo nchini kwani aina nyingi zinazoagizwa kutoka nje zina virutubisho visivyo sahihi vilivyotengenezwa kwa udongo wa Ulaya na Amerika Kaskazini.

Mwaka jana, Rais William Ruto alisema utawala wake utaagiza magunia milioni sita ya mbolea kabla ya mvua ndefu inayoanza Machi.

Kwa muda mrefu, Bw Linturi alisema, serikali inanuia kuwekeza katika uzalishaji wa mbolea ili kupunguza gharama ya juu ya uzalishaji wa chakula nchini.

“Kuwa na kiwanda cha kutengeneza mbolea kuna uwezekano wa kuchochea uzalishaji wa kilimo kwa kupunguza bei ya ununuzi wa pembejeo muhimu za kilimo, na hivyo kusababisha kupungua kwa gharama ya uzalishaji wa chakula,” alisema.

Kwa sasa, nchi inategemea sana uagizaji wa mbolea kutoka nje kwani majaribio mbalimbali ya kuanzisha kiwanda cha kutengeneza mbolea yamekuwa na matokeo kutokana na sababu mbalimbali.

MANCHESTER UNITED VS NOTTINGHAM FOREST 

manchester

Mabao ya kipindi cha pili kutoka kwa Anthony Martial na Fred yalihakikisha ushindi kwa vijana wa Erik ten Hag usiku huo, ingawa nafasi ya kuingia fainali ilikuwa salama kutokana na ushindi wao wa 3-0 wa mkondo wa kwanza kwenye Uwanja wa City Ground.Read More

Martial akifunga bao lake la sita msimu huu baada ya pasi iliyokusudiwa kwa Marcus Rashford kurudi kwa mshambuliaji huyo wa Ufaransa dakika 17 kabla ya mchezo kumalizika.

Ndani ya sekunde 180, United walipata bao lingine wakati Bruno Fernandes alipomwekea Rashford pasi maridadi ya mpira wa krosi, ambayo Muingereza huyo alielekeza kwa Fred, ambaye aliukwamisha mpira kwenye wavu tupu kwa kutumia goti lake.

Mchezaji mpya aliyesajiliwa Marcel Sabitzer alifuatilia mchuano huo kwa makini wakati United ikijiweka kwenye hatua ya ushindi wa kombe lao la kwanza tangu 2017. 

Ingawa mbio zao bila kupata mabao hazilingani na zile za Newcastle, United wanajua kwamba ikiwa watakosa kuchukua kombe msimu huu itakuwa ni muda mrefu zaidi kwa klabu hiyo kupata fedha tangu walipopata ubingwa wa Ulaya mwaka 1968.

 

STANDARD RADIO IMETEMBELEWA NA UGENI KUTOKA UBALOZI WA MAREKANI TAREHE 5 NOVEMBER 2019.

IMG_4214

IMG_4210

STANDARD RADIO IMETEMBELEWA NA UGENI KUTOKA UBALOZI WA IRELAND.

IMG-20180524-WA0004
ugeni huo ulimjumuisha balaozi wa Ireland, wabunge kutoka Ireland na mkuu wa wilaya ya Singida
IMG-20180524-WA0007
pia wageni waliomba kutembelea studio za standard radio
IMG-20180524-WA0013

BACKGROUND

The Standard Radio is a registered company in the United Republic of Tanzania bearing the incorporation registration number 81651 of 2011. Standard Voice Limited is the brain child of Mr. James Japhet Daud an entrepreneur who has the zeal of bringing positive changes to the people of Singida. Under the umbrella of Standard Voice Limited, Standard Radio came to life in 2012 September and since then it has been educating, entertaining and informing Singida and its environs with development oriented content.

Meet their development goals and other community and social activities to the citizens of the United Republic of Tanzania and beyond via Radio Broadcasting. This we have started to do with the central and western zone Standard Radio Fm 90.1 is devoted to helping the community keep track of the development agenda by acting as a conveyor belt to attaining this dream.. As a member of the fourth estate, we shall engage in objective, ethical and professional reporting to ensure that we serve the interest of the people.

Standard Radio Fm 90.1 is available in Singida and its environs. In our strategic plan, Standard Radio Fm 90.1 will be a national radio station serving the people of Tanzania on satellite and internet broadcasting platforms.

VISION

“To be the best Radio in Tanzania which will provide comprehensive, balanced and objective coverage of issues  at  local, regional, national and international levels”

VOICE OF THE VOICELESS:

As our slogan states, our mission is to serve as a bridge to local community and the local and central government and any institution that has the same goal as us for example the NGOs, so we are talking about the Voiceless we mean that, people are living in different challenges, so our objectives are sticking on the local community development Agenda.

MISSION

“To be the bridge and centre that will empower its listeners to articulate their concerns and to mobilize them for community, economic development through small, medium and large entrepreneurship from the village up to the national level”

The Standard Radio operates an effective, sustainable and community owned radio that champion development within and around its footprint. To strive for visible and measurable community support and ensure that programming content reflects community demographics, needs and priorities.

HomeAbout UsOur TeamContact
© 2015 All rights reserved Standard Voice Limited..Developed by Powerweb